IVECO TRAKKER YENYE GIA BOKSI YA EUROTRONIC ILIYOANZISHWA NA SMAG

Iveco ilionyesha Iveco Trakker EuroTronic Dubai. Tukio la uanzilishi lilihudhuriwa vizuri sana, likivutia machapishi maalum makuu na zaidi ya wateja 150 kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwakilisha manispaa, biashara za ujenzi,machimbo, waendeshaji usafiri na watenda kazi wengine waliovutiwa na kizazi cha chapa cha hivi karibuni zaidi cha magari ya nje ya barabara kwa kazi ngumu mno za nje ya barabara. 

Tukio hili, lilopangwa na msambazaji wa Iveco Saeed Mohammed Al Ghandi &Wana (SMAG) kwenye Dubai Autodrome, lilitumia vizuri mno vituo kuonyesha mkusanyiko mkubwa wa Trakker. Waliojihusisha pia walikuwa na fursa ya kupitia utulivu murwa zaidi wa kabu na utenda kazi wa uendeshaji wa gari hili kwenye njia ya mashindano ya Autodrome.

Aina za Trakker zilizochaguliwa zilikuwa kwenye maonyesho, ikionyesha kunyumbulika kamili kwa mkusanyiko huu, kiasili modeli kwa kila shughuli.Nyota ya uanzilishi, Trakker EuroTronic, iliwekwa kando ya modeli nne za Trakker AD380 zenye miundo tofauti: tipa, kompakta, tanka la maji na kichanganya. Bidhaa kama hizi pia ilikuwa zinapatikana kwa majaribio ya uendeshaji.

Sio tu Trakker iliyokuwa kwenye maonyesho na majaribio ya kuendeshwa, kwa kweli tukio hili lilikuwa nafasi ya kuonyesha orodha yote ya Iveco ikiwemo mkusanyiko wa magari wastani na yasiyo mazito, pamoja na Eurocargo na Daily kwenye miundo tofauti.

Trakker ilibuniwa kukidhi mahitaji ya wateja ya nguvu na kuaminika kwenye kazi barabarani na zisizo barabarani ikiwa na Uzito wa Gari wa Jumla unaoania kutoka tani 18 hadi 70 na Uzito wa Mchaganyo wa Jumla wa tani 41 hadi tani 70.                                                                                                                                                               
Ubunifu wa kweli wa Trakker mpya ni kabini ya asili ya Stralis inayotoa kiwango cha utulivu barabarani kinachohusishwa na utendaji kazi wa nje ya barabara.

Gia boksi ya kujiendesha ya EuroTronic inatoa faida zenye maana. Inaweza kutumika kwenye mtindo wa kujiendesha kamili au nusu.Shifti ya gia ya kujiendesha inapigiwa hesabu kulingana na hali ya mzigo, hali ya barabara na mtindo wa uendeshaji. Ili utendaji kazi wa gari, matumizi ya fueli na utulivu uboreshwe. Upesi wa gia unalinganishwa kwa kukubaliana kielektroniki na upesi wa injini, ni haraka zaidi kuliko kulinganishwa kwa msuguano. Hii ni nzuri kwa maeneo ya ujenzi ambayo gari linalazimika kupanda kwa ajili kukosa upesi huwa ni kidogo. Ikiwa dereva anataka kubakisha uwiano huohuo kwenye njia ngumu, anaweza kuswichi kwa mtindo wa kujiendesha nusu kudhibiti mabadiliko ya gia. Na EuroTronic, dereva anaweza kujimakini kikamili na uendeshaji, hakuna haja ya kuondoa mikono kwenye usukani, na gari linatenda kazi vyema kabisa wakati wote. Matokeo ni utulivu wa hali ya juu na kupunguza kuchoka kwa dereva, pia ufanisi wa fueli mzuri na gharama za matumizi ndogo, kivingine, usalama na faida.

Kwa uingizaji wa gia boksi ya Eurotronic, mkusanyiko wa Trakker ni mpana kuliko kitambo, ukijivunia utoaji bidhaa unaowaruhusu wateja kulenga bidhaa kwa kazi maalum. Mkusanyiko unajumuisha injini za Cursor 13 na kabini 2  (Hi-Land and Hi-Track). Matoleo ya malori madhubuti yanapatikana kwa miundo ya 4x2, 4x4, 6x4, 6x6, 8x4 na 8x8 ikiwa na vipimo vya nguvu vya kutoka 380 hadi 440hp. Matoleo ya trakta yanapatikana kwa miundo ya 4x2, 4x4, 6x4 na 6x6 ikiwa na vipimo vya nguvu kutoka 380 hadi 440hp.